KAMATI YA SIASA YA CHA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.
Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Morogoro ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Gerlod F Mlenge , Januari 4 Hadi 5 2025 imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Miradi iliyokaguliwa imejumuisha sekta za Elimu, Afya, Maji na Miundombinu ya Barabara.Kamati ya Siasa ya Wilaya imetoa maelekezo na mapendekezo Kwa wasimamizi wote wa Miradi kuhakikisha Miradi inatekelezwa Kwa wakati, na haitosita kuwawajibisha wote watakaobainika kukwamisha Miradi ya Maendeleo.
Akikagua Miradi,Mwenyekiti wa CCM Wilaya Mh Gerlod F Mlenge amewataka wasimamizi wote wa Miradi kuhakikisha inakamilika Kwa wakati.
" Mheshimiwa Rais anatoa fedha nyingi sana Katika Miradi mbalimbali kuhakikisha wananchi wanapata huduma, msimkwamishe tafadhali kwani Kumkwamisha Mheshimiwa Rais ni kukikwamisha Chama Cha Mapinduzi.
Hivyo wale wote mliopewa dhamana ya usimamizi wa Miradi hakikisheni inakamilika na Kutoa huduma" amesema Mlenge.
Ziara hiyo ya siku mbili imelenga kukagua Miradi ya Maendeleo na kuhakikisha inakwenda sambamba na thamani ya Fedha inayotolewa na Serikali ya Awamu ya sita.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.