Kamati ya Siasa ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imefurahishwa na Kikundi cha Wanawake UMAKI kilichopo Dutumi.
Akiongea na Kikundi hiko (UMAKI) leo Novemba 16, 2023 Ndg. Gerorld Mlenga amewapongeza UMAKI Kwa kuonesha bidii na matumizi Bora ya fedha walizokopeshwa na Halmashauri.
"Nimefarijika sana Kikundi ambacho kinajitambua, kinakopa kinarejesha... na nitasikitikasana kama itafika mahali nitaona hamuwafanyii muendelezo kwa sababu wanaonekana wanajali maendeleo na wanafanya mambo yanayooneka kwa macho. UMAKI oyeee..!" alisema Ndg Mlenga.
Nae Mhe. Rebeca Nsemwa, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro aliwasihi wafanye kilimo kilicho Bora zaidi na Cha kisasa na kwamba atawaunganisha na wataalam wa SUA Kwa msaada na ushauri Bora zaidi wa Kilimo.
"Yaani mie nataman Kikundi hiki niwe natembea nacho kuwafundisha Wanawake wengine au vikundi vingine" alisisitiza Mhe. Rebeca
Kamati hiyo ya siasa imefanya ziara yake leo kutembelea na kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ikiwepo madarasa na mabweni Matombo sekondari ambapo ilipata wasaa wakuongea na wanafunzi(wasichana) wa kidato cha Tano, pia ilitembelea miradi ya Maji (wa Morong'anya-Madamu, na Maji mserereko-Mvuha), mradi wa birika la kunywenyea mifugo-Dakawa, mradi wa barabara Gomero-Nyarutanga na ujenzi wa daraja Vihengere-Lundi, na Kikundi vya ujasiliamali UMAKI-Ditumi na JEMBE MALI-Bwakira
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.