Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima amemkaribisha Ndg. Mathias Kabunduguru ambaye ameteuliwa kuwa Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu kujiunga na Timu ya Wizara katika kufanikisha shughuli za maendeleo ya wananchi.
Akimkaribisha leo katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zilizoko Mtumba Jijini Dodoma Dkt. Gwajima amesema watumishi wa TAMISEMI wanaushirikiano wa hali ya juu na watakuwezesha kufanikisha majuku yako.
“Karibu tuchape kazi ya kuwahudumia wananchi, kwetu ni kazi tu; Sina shaka na wewe kwa kuwa ni mwalimu wangu na ulinipokea katika utumishi wa umma hivyo nakukaribisha TAMISEMI ya wananchi hivyo karibu tuwahudumie na kuwatumikia watanzania”Amesema Dkt. Gwajima.
Amewapongeza watumishi kwa weledi waliouonyesha kwa kipindi chote cha Uongozi wa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Ndg. Tixon Nzunda katika Wizara hii mpaka alipoteuliwa na kuwa Katibu Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu.
“Tumepata faraja kubwa sana kwa Ndg. Nzunda kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu na mafanikio haya ni yetu sote kwani tumefanya naye kazi nzuri zilizopelekea kuteuliwa katika nafasi ya juu zaidi ninawapongeza watumishi wote wa TAMISEMI na ninawasihi muendeleze na kazi hii nzuri kwa Naibu Katibu Mkuu (Elimu) Ndg. Mathias Kabundunguru” Amesema Dkt. Gwajima.
Naye Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia elimu Ndg. Kabunduguru amewataka watumishi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu za kazi zinavyotaka ili kuhakikisha wanatimiza adhima ya kuleta matokeo bora ya maendeleo kwa watanzania na nchi kwa ujumla.
Ndg. Kabunduguru amesema kuwa kila mmoja anawajibu wa kuheshimu kazi muda wote ili kuweza kupata matokeo chanya ambayo msingi wake ni utii wa sheria,kanuni na taratibu za kazi ili kufanyikisha malengo yanayotakiwa kwa watanzania.
“Na ili kufanikiwa kufikia malengo hayo lazima tushirikiane kwa mimi kujifunza kutoka kwenu na nyinyi kujifunza nini nilicho nacho ili kufikia adhima yetu ya kujenga taifa moja kwani sote lengo letu ni moja” Ameeleza Ndg. Kabunduguru
Naye Katibu Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu. Mhe.Tixson Nzunda amewashukuru watumishi wa OR-TAMISEMI kwa ushirikiano waliyompa kipindi chote alipokuwa akifanya nao kazi na kutaka kuendelea kutoa ushirikiano kwa Ndg. Kabunduguru ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake kwa ufasaha.
Aidha ikumbukwe kabla ya uteuzi wa hivi karibuni Ndg. Kabunduguru alikuwa Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Ndg. Nzunda alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu.
Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.