Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ismail Ally Ussi ameonyesha kuridhishwa na kupongeza usimamizi na Utekelezaji wa Miradi iliyotepitiwa na Mwenge wa Uhuru Katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
"Mwenge wa Uhuru umeridhishwa na Utekelezaji wa Miradi wilayani hapa,muendelee kuitunza Miradi hii maana imetekelezwa Kwa gharama ya Fedha nyingi, Kwa kufanya hivyo tutakua tunalitendea haki Taifa na kuunga mikono juhudi zinazofanywa na Kiongozi wetu Mheshimiwa DKt.Samia Suluhu Hassan zakuwaletea wananchi maendeleo" Alisema Ussi
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Ndugu Jeshi Godfrey Lupembe akikabidhi Mwenge Kwa ndugu Emmanuel Mkongo Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Morogoro kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Musa Kilakala amesema, kama Halmashauri wameyapokea maagizo yote yaliyotolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge na kuahidi kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo.
"Kiongozi wa mbio za Mwenge tunakushukuru sana Kwa kutembelea,Kukagua na kuzindua Miradi takribani Tisa kama Halmashauri tunakuahidi kuyafanyia kazi maelekezo na maagizo yako haraka iwezekanavyo" Alisema Lupembe.
Miradi iliyopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru ni Mradi wa maji Kijiji Cha Diguzi, Mradi wa Soko Ngerengere,Kikundi Cha ufugaji Ngerengere, Zahanati ya Gwata,Mnada wa Mifugo Gwata, Kiwanda Cha nguzo za umeme za zege Fulwe, Ujenzi wa vyumba vya madrasa na vyoo Sekondari ya Fulwe,Ujenzi wa Kalavati kungwe tomondo na Mradi wa Nishati safi ya kupikia Mikese ambayo yote Kwa Pamoja inathamani ya Shilingi bilioni 4.4 za kitanzania.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.