Maafisa ugani wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro kwa furaha wamemshukuru rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania mh.Dk Samia Suluhu Hasani kwa kuwapatia vitendea kazi vya kidigitali ikiwa ni vishwambi na magwanda ya kilimo kwa lengo la kilimo chenye tija.
Maafisa ugani hawa wamekabidhiwa jumla ya vishikwambi 77 na magwanda 79 na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ndg. Lucas Lemomo leo katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri uliopo Mvuha na kuwataka kutumia vitendea kazi hivi katika ukusanyaji wa mapato, kuwqsajili wakulima kwenye mifumo ya pembejeo kwa msimu husika na kwa ufanisi, na kuhakikisha upatikanaji na usambazaji wa taarifa muhimu za shughuli za ugani zinapatikana kwa wakati.
"Hakikisheni vitendeakazi hivi vinaleta tija na mabadiliko katika uchumi wa mkulima mmojammoja na kuiongezea halmashauri mapato kupitia kilimo cha kidigitali" amesisitiza mwenyekiti Lemomo.
Vitendea kazi vitamsaidia mkulima kusajiliwa kwenye mfumo, kuchukua matukio shambani, upatikanaji na utoaji wa elimu kwa njia ya video na kurahisisha usambazaji wa teknolojiaza kisasana kilimo mashambani na mwisho kutumia kupima na kupata ukubwa wa mashamba kupitia programu na mdumo wa GPS.
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.