Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro inaendelea na kazi ya uandaaji wa mpango wa bajeti kwa kipindi cha mwaka wa fedha2019 /2020
Kazi hiyo inaendea katika ukumbi wa Halmashauri chini ya Afisa Mipango wa wilaya Bw Elias Salifu. Akizungumzia kazi hiyo afisa mipango amesema kuwa
Bw Elias Salifu amesema uandaaji wa mpango wa bajeti kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2019/ 2020 ni kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli zote za Halmashauri. Alisema kuwa Maandalizi ya bajeti yanafanyika kwa kuzingangatia mwongozo wa bajeti wa mwaka 2019/2020, Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2015-2020), Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano, Mpango wa Taifa wa Maendeleo Endelevu, Miongozo mbalimbali ya Kisekta pamoja na kuzingatia Vipaumbele vya Wananchi.
Bw. Salifu aliendelea kusema kuwa Katika Bajeti hii, Halmashauri imepanga kukusanya na kutumia Jumla ya Tsh. 42,625,824,024.50 ambapo kati ya kiasi hicho, Kiasi cha Tshs. 2,201,584,000.00 kitakusanywa kutoka Vyanzo vya ndani sawa na asilimia 5.2 ya Bajeti iliyopangwa
Bajeti ni uti wa mgongo katika mwelekeo wa utendaji kazi za Halmashauri na kupanga namna kazi zitakavyotekekelezwa katika mwaka mmoja.
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.