Mradi wa Kuleta Mageuzi katika sekta ya makaa Tanzania umeendesha warsha kwa madiwani wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro katika ukumbi wa Oasis Mjini Morogoro.
Semina hiyo imehudhuriwa na madiwani wote wanaowakilisha kata zote pamoja na madiwani wa viti maalum pamoja na baadhi ya wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri. Wataalamu mbalimbali wa Mradi wa TTCS walitoa mada wakiwepo Meneja Mradi TTCS Charles Leornard, Bettie Luwuge na wengine wengi.
Mada mbalimbali zilitolewa na kujadiliwa katika warsha hiyo vikiwemo hali ya uharibifu wa misitu kitaifa, fursa zilizopo katika misitu, malengo ya mradi wa TTCS, Matokeo ya utafiti wa kuangalia viwango vya uchipuaji wa misitu baada ya misitu kuvunwa kwa ajili ya uzalishaji mkaa chini ya mapango wa usimamizi shirikishi wa vijiji.
Mradi huu upo katika vijiji 30 katika mkoa wa Morogoro, Katika Halmashauri ya Morogoro vipo vijiji vitano vilivyopata mradi ambavyo ni Diguzi, Matuli, Lulongwe na Mlilinga. Kijiji cha tano bado hakijachaguliwa taratibu za kukipata bado zinaendelea.
Pamoja na faida kubwa ya kipato wanayoipata wananchi waliojiunga katika vikundi na kupata mafunzo katika kuhifadhi msitu na kuzalisha mkaa chini ya mradi huu, mradi huu pia una faida kubwa kwa jamii husika kwani huwezesha kujengwa kwa ofisi za vijiji, madarasa,zahanati, isim virefu vya maji pamoja na barabara kutokana na mapato yanayopatikana katika kijiji.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.