Viongozi wa Mkoa wa Morogoro na Wilaya zake wakifuatilia mawasilisho ya taarifa mbalimbali katika Kikao kazi cha Viongozi wa Mikoa na Wilaya kwa njia ya mtandao kuhusu maendeleo ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.
Kikao hicho kimefanyika leo februari 18, 2022 ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ndio Mwenyekiti wa Kikao hicho.
Akifungua kikao hicho Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewapongeza Wakuu wa Mikoa na Wilaya kwa kuendelea kufuatilia miradi ya maendeleo kwa ukaribu na hasa amewapongeza kwa kufanikisha ujenzi wa miradi iliyotokana na fedha za Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Kati ya mambo mengi yaliyojadiliwa ni pamoja na taarifa zilizowasilishwa ambazo ni hali ya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, hali ya maandalizi ya Sensa ya majengo na hali ya maandalizi ya sensa ya Anwani za Makazi.
Serikali inaendelea na maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi na wakati huohuo zoezi la Mfumo wa Anwani za Makazi unaendelea, Serikali inaendelea kuwaomba Wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali wakati mazezi hayo yakitekelezwa.
#Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.