Mufti wa Tanzania Dkt Sheikh Abubakar Zuberi bin Ally aongoza mamia kumzika aliyekua Kadhi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Sheikh Musa Bolingo aliyefariki Dunia 27 Disemba 2024 majira ya saa Moja jioni.
Akitoa salamu za msiba Kwa waombolezaji Mufti amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan Kwa kugharamia msiba huo, huku akisema wamempoteza kiongozi mahiri.
"Tunachoweza kusema tumempoteza mwanazuoni mchapakazi na kiongozi mahiri na mkombozi wa Mkoa wetu wa Morogoro" Alisema Mufti Abubakar
Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mheshimiwa Adam Kighoma Malima akitoa salamu za pole aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu kuhakikisha wanaweka jitihada katika elimu zote ikiwema elimu Dunia na Elimu ya dini kwani zitawasaidi hapa duniani na baada ya kutoweka hapa duniani.
Naye Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Musa Kilakala akitoa salamu Kwa waombolezaji amesema Katika vitu ambavyo mwanadamu anapaswa kufahamu kuwa ni vya Uhakika ni Kifo.
"Ndugu zangu Kifo ni jambo la Uhakika, hivyo tunapaswa kuhakikisha tunajiandaa Kwa kutenda matendo mema" Alisema Kilakala
Mbunge wa Morogoro mjini Mheshimiwa Abdullazizi Abood,akitoa salamu za pole amesema Sheikh Bolingo alikuwa mpenda maendeleo hususani Shughuli za kijamii kama Afya na Elimu ambapo ameahidi kutimiza ahadi yake Katika kuikamilisha Ujenzi wa Zahanati ambayo Marehemu Sheikh Bolingo alikuwa ameianzisha.
Marehemu Sheikh Musa Bolingo amezikwa 28 Disemba 2024 Katika msikiti wa Luqman uliopo Kihonda majira ya saa kumi baada ya kuswaliwa ibada iliyoongozwa na Mufti Abubakar Zuberi bin Ally.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.