Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameuagiza Uogozi wa Maonyesho ya nanenane Kanda ya Mashariki kuhakikisha Taasisi zote za kilimo, mifugo na Uvuvi zinafanya shughuli zao katika Uwanja wa maonesho wa Nanenane kanda ya Mashariki mwaka mzima badala ya kusubiri kipindi cha maonesho hayo pekee.
Makamu wa Rais ametoa agizo hilo leo Agosti 8, mjini Morogoro wakati anafunga rasmi maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Maarufu kama Nane nane Kanda ya mshariki yaliofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjini Morogoro.
Makamu huyo wa Rais aliwaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya zilizopo katika Kanda hiyo kusimamia usalama wa chakula kwa kuweka msisitizo kwa wakulima kufanya kilimo biashara na sio kuwataka wabaki na vyakula ndani pekee.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen Kebwe amesema Mkoa umejiwekea lengo la kuhakikisha wanafikia kulima hekta laki tisa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuendelea kulima mazao ya kimkakati.
MWISHO.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.