Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dkt. Kusirye B. Ukio ameutaka Uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Morogoro kuhakikisha unasimamia dawa ipasavyo katika Hospitali hiyo.
Dkt. Kusirye B. Ukio ameyasema hayo leo Oktoba 28, 2021 alipotembelea kambi ya Macho inayoendelea kutoa huduma ya matibabu ya macho katika Hospitali ya Wilaya ya Morogoro (Mvuha).
Katika hatua nyingine Dkt. Kusirye B. Ukio amesema kuwa ameridhishwa na mwitikio wa Wananchi kujitokeza kupata vipimo na matibabu ya macho na kuutaka Uongozi wa Hospitali hiyo kuweka mikakati ya kufanya huduma hiyo kuwa endelevu mara baada ya mradi huu wa Boresha macho unawezeshwa na Shirika la Sight savers utakapofikia ukomo wake.
Huduma hii ya macho imeanza kutolewa jumatatu ya tarehe 25 na kufikia tamati kesho ijumaa ya tarehe 29/10/2021 kwa awamu hii.
#boreshaMacho
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.