Mkuu wa Wilaya Mh. Musa Kilakala ameongoza matembezi ya kuhamasisha wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Matembezi hayo yamefanyika katika uwanja wa Njia nne uliopo kata ya Ngerengere, yenye urefu wa kilomita tano (5km) kuanzia saa 12:45 asubuhi mpaka saa 1:45 asubuhi. Matembezi hayo yamehitimishwa na hotuba iliyolenga kuhamasisha wananchi kujitokeza Katika zoezi la kupiga kura kuchagua Viongozi wa Serikali za Mitaa wanaowataka Ili kuwaletea maendeleo na kuwajibika katika vijiji na vitongoji vyao.
" Hongereni sana wanangerenge na wote mliojitokeza Katika matembezi haya, niwaombe kila mwenye miaka 18 na kuendelea na amejiandikisha kwenye daftari la Mpiga kura ahakikishe anajitokeza kwenda kupiga kura kwa wingi kama mliojitokeza Leo kwenye matembezi haya". Amesema Mhe. Kilakala.
Vilevile, matembezi hayo yalihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. Lucas Lemomo ambaye aliwataka wananchi kujitokeza kupiga kura ifikapo tarehe 27-11-2024 kwani hutokea kila baada ya miaka mitano hivyo ni muhimu kufanya maamuzi na kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo .
Aidha, matembezi haya yameambatana na zoezi la uchangiaji wa damu salama lililotatibiwa na hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro. (MDH).
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.