Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Rehema S. Bwasi amewaagiza walimu wakuu na wakuu wa shule wanaosimamia miradi ya vyumba vya madarasa na maabala katika shule zao na Watendaji wa Vijiji vyenye miradi ya Zahanati kumaliza ujenzi hadi kufikia Mei 15, 2021 na atakaekuwa hajamaliza atachukuliwa hatua.
Bi. Rehema S. Bwasi ameyazungumza hayo jana Juni 1, 2021 katika Kikao Kazi cha ukamilishaji wa Miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashari ya Wilaya ya Morogoro ambapo jumla ya madarasa 20, maabala 12 na Zahanati 7 zinaendelea kujengwa.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi amewataka wasimamizi hao kutoleta ujanja ujanja na upigaji kwenye manunuzi huku akisisitiza matumizi mazuri ya fedha hizo ili miradi ikamilike, "Nimeshawarudisha sio watatu au wanne waliokuja na bei zao za ajabu na baada ya kuwarudisha wakawa wameokoa zaidi ya milioni sita, narudia tena ukija na bei zako za ajabu nitakurudisha."
Walimu wakuu hao, wakuu wa shule na Maafisa Watendaji wa Vijiji wametakiwa kufanya kazi usiku na mcchana na kutakiwa kumaliza kazi hadi kufikia Mei 15, 2021.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.