Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Bi Rehema Saidi Bwasi amewapokea waalimu 20 walioripoti kwa ajili ya kufanya kazi katika Halmashauri ya wilaya ya Morogoro. Akiwakaribisha kufanya kazi katika Halmashauri hiyo katika kikao alichokifanya na watumishi hao katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Morogoro uliopo Mvuha, Mkurugenzi Mtendaji amewaasa waalimu hao kuwa hodari katika utendaji kazi pamoja na kuwa raia wema katika maeneo wanayokwenda kuanza kazi na kuzingatia sheria na taratibu za utendaji wa kazi.
Amewaasa waalimu hao kutoa huduma bora kama kanuni za utumishi wa umma zinavyotaka
Kufanya kazi kwa bidii kwa kujitoa, Kutoa huduma bila ya upendeleo, Kufanya kazi kwa uadilifu
Waalimu hao ambao tayari wamekwisha pangiwa vituo vyao vya kazi ni wa shule za msingi na sekondari.
Akiwafafanulia waajiriwa wapya Afisa Utumishi Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Ndg Kelvin Luviga amwasisitizia waalimu hao juu ya kuzingatia sheria za utumishi wa umma
popote wanapokuwa katika kutekeleza majukumu yao na hata nje ya vituo vyao kazi.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.