Mkurugenzi wa vijana ajira na watu wenye ulemavu Ndugu Juma Abrahamani ameeleza kuvutiwa na miradi ya Vijana na walemavu katika Halmashauri ya Morogoro. Akiwa katika ziara ya kutembelea Vikundi vya Vijana na wallemavu wilayani hapa Ndg Juma aliweza kutembelea miradi mbalimbali inayoendeshwa na vijana wilayani hapa siku ya Jumamosi tarehe 15/6/2019
Aliweza kutembelea mradi wa Kufyatua matofali eneo la Kijiji cha Dala Kata ya Mvuha, Ghala la kuhifadhia nafaka kijiji cha Mbwade kata ya Bwakila chini, kutembelea eneo la uwekezaji la utalii Majimoto Kisaki.
Katika hotuba yake alielezea kuridhishwa na utekelezaji wa asilimia nne za vijana katika Halmashauri ya Morogoro na pia aliwasisitiza vijana kutunza mradi, kufanya kazi kwa bidii pamoja na kurejesha fedha na wizara haitosita kuwasaidia katika kuboredsha mchakato wa kuongeza thamani katika miradi yao.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.