Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Kebwe Stephen Kebwe amefanya ziara ya Kushtukiza na kupita kwenye maghala ya kuhifadhia mafuta ya kula na sukari katika Manispaa ya Morogoro kwa ajili ya kukagua wafanyabiashara wanaoficha bidhaa hiyo.
Dk. Kebwe amefanya ziara hiyo Mei 15, mwaka huu akiambatana na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na kujionea maghala mengi yakiwa yamejaa mafuta ya kula na kuwataka wafanyabiashara kutoficha bidhaa hizo badala yake wazipeleke sokoni kwa ajili ya kuuza kwa wananchi kwa bei elekezi ya Serikali.
Katika ziara hiyo Dkt. Kebwe ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, amemuagiza Kamada wa Polisi wa Mkoa pamoja na Maafisa wa TRA wa Mkoa huo kumchukua na kumhoji Mfanyabiashara maarufu wa Mafuta ya kula Hussein Bionzo na kuzipitia nyaraka zake za biashara hiyo ili kujiridhisha endapo analipa kodi serikalini.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.