Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa Vituo vya afya na Hospitali ya wilaya inayojengwa eneo la Mvuha yalipo Mkao makuu ya wilaya hii.
Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ameagiza Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kuhakikisha majengo yote ya Hospitali ya wilaya kuwa yameezekwa ifikapo Julai 15, mwaka huu.
Dkt. Kebwe alifanya ziara hiyo Juni 19 mwaka huu wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Halmashauri hii.
Pamoja na agizo hilo Dr. Kebwe ameagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kumsimamia Afisa manunuzi wa wilaya ili aweze kununua vifaa vya Ujenzi kwa wakati. Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ipo katika ujenzi wa majengo mapya katika kata ya Mkuyuni, Duthumi pamoja na Matombo. Ujenzi wa majengo ya Duthumi na Mkuyuni upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wakati ujenzi wa majengo ya kituo cha kisemu utaanza hivi karibuni, kwa sasa eneo la ujenzi lipo katika hatua ya usafishwaji.
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.