Leo Oktoba 21, 2021 timu ya wataalamu wa Halmashauri ikiongozwa na Mhandisi Juma Chimwaga imepita katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri kukagua maeneo yatakayojengwa madarasa mapya ambayo yemetengewa fedha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Katika mgao wa fedha kupitia Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imenufaika kwa kupata madarasa 103 kwa ajili ya shule za Sekondari yenye thamani ya fedha za Kitanzania Bilioni 2 na Milioni 60, pia Halmashauri imepata mgao wa madarasa 11 kwa shule shikizi 5 za Msingi kwa thamani ya fedha za Kitanzania Milioni 220, wakati huohuo Halmashauri imenufaika kwa mgao wa fedha kwa ajili ya kuanzisha huduma za dharula katika Hospitali ya Wilaya yenye thamani ya fedha za Kitanzania Milioni 300 na nyumba ya watumishi wa Afya yenye thamani ya fedha za Kitanzania Milioni 90.
Taratibu za ujenzi wa miradi yote hiyo imeshaanza na itafanyika kwa haraka ili kufikia Januari 2022 wanafunzi wa Kidato cha kwanza wataanza kuyatumia madarasa hayo na timu imeshaanza kupita kukagua maeneo rasmi yaliyoandaliwa kwa ujenzi wa miradi hiyo ili ujenzi huo uanze mara moja.
#AsanteRaisSamiaSuluhuHassan
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.