• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Morogoro District Council
Morogoro District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Afya
      • Maji
      • Utawala na Utumishi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Utalii
    • Vivutio vya Utalii
      • Msitu wa Pangawe
      • Msitu wa Milawilila
      • Msitu wa Kimboza
      • Maji Moto-Kisaki
      • Kisimbi-Kinole
      • Utalii Matombo
    • Maeneo ya Kihistoria
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Huduma za Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MOROGORO YAPONGEZWA KAMPENI YA JISOMESHE NA MKARAFUU

Imetolewa: February 17th, 2025

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara,  kilimo na Mifugo  Mhe. Deo Mwanyika (MB) ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Morogoro chini ya Mkuu wa Mkoa huo Adam Kighoma Malima kwa kuja na ubunifu wa kampeni ya "Jisomeshe na Mkarafuu" ambayo itaenda kuinua kipato cha wanafunzi na kuweza kupata mahitaji yao ya msingi ikiwemo Elimu. 


Mhe. Mwanyika ametoa pongezi hizo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya JISOMESHE NA MKARAFUU iliyozinduliwa katika Kata ya Mkuyuni Mkoani humo kwa kuwapatia wanafunzi 800 wa kidato cha kwanza miche 10 kila mmoja ili iweze  kuwasaidia wanafunzi hao katika maisha yao ya baadae hususan katika safari yao ya Elimu kwa kulima zao hilo la karafuu. 


Mhe. Mwanyika amesema, Serikali ya Mkoa wa Morogoro kupitia Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima imechukua maono ya Mhe. Rais na Wizara ya kuhakikisha na kutekeleza agenda ya kilimo ifikapo 2030, pia kuhakikisha bei elekezi ya mazao ya viungo yanasimamiwa ipasavyo ili kuwainua wananchi kiuchumi. 


"Nakupongeza sana Mhe. Mkuu wa Mkoa huu ni ubunifu mkubwa na mimi niseme tu ukweli hapo nitaiga" amesema Mhe. Deo Mwanyika. 


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema kuna umuhimu wa kuongeza elimu ya ugani kwa wazazi ili kuondokana na changamoto ya kufa kwa baadhi ya miche ya karafuu huku akitoa ahadi kwa Mhe. Rais kuwa ndani ya miaka mitano  Mkoa wa Morogoro utakuwa eneo la uzalishaji namba mbili wa karafuu duniani. 


Naye Katibu Tawala wa Mkoa huo Dkt. Mussa Ali Mussa akielezea umuhimu wa kampeni hiyo amesema kampeni hiyo inalenga wanafunzi wa kidato cha kwanza  kupanda miche hiyo ili kuwasaidia wanafunzi hao kujisomesha wenyewe kupitia zao la karafuu kwa kuuza karafuu hivyo pia  kukuza uchumi wa familia zao,  Mkoa na Taifa kwa ujumla na ututunzaji wa mazingira. 


Naye Pascal Petro Gabriel mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya Sekondari ya Mkuyuni amesema wameipokea kwa moyo mmoja kampeni hiyo na kwamba miche hiyo itawasaidia kipindi cha masomo na hata baada ya masomo. 


Baada ya uzinduzi wa Kampeni ya JISOMESHE NA MKARAFUU katika kata ya Mkuyuni Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Kamati ya Bunge ya Viwanda Biashara kilimo na Mifugo iliendelea na ziara yake ya kukagua shughuli za kilimo katika Kata ya Tawa, ziara hiyo inaendelea Februari 18, 2025 katika Wilaya ya Kilosa na Kilombero. 


MWISHO.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 15, 2024
  • TANGAZO A UPANGA VYUMBA VYA OFISI NA MAENEO MBALIMBALI YALIYOPO MOROGORO MJINI March 19, 2025
  • TANGAZO LA KAZI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU, DEREVA NA MTENDAJI WA KIJIJI July 15, 2024
  • TANGAZO LA RASIMU July 25, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi karibuni

  • KIONGOZI MBIO ZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI ILIYOPITIWA NA MWENGE WA UHURU 2025

    April 12, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEEA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO,MAAGIZO YATOLEWA

    April 11, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA MOROGORO AENDELEZA KAMPENI YA JISOMESHE NA MKARAFU

    March 14, 2025
  • "BAINISHENI VYANZO VYA MAJI NA MVILINDE" MHE.KASSIM MAJALIWA MAJALIWA

    March 05, 2025
  • Angalia zote

Video

Mfumo wa Mikopo ya 10% Namna ya Kujisajili
Vidio Zaidi

Kurasa za haraka

  • Sheria ya Manunuzi ya umma
  • Sheria ya Ardhi

Tovuti nyingine

  • Salary Slip Self Service
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani yake

Wasiliana nasi

    Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road

    Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania

    Simu: +255 23 2935458

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.