Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM-mkoa Mh. Hamza Mfaume leo October 5, 2014, amekabidhi zawadi kwa washindi wa Mvuha Tounerment Cup 2024 katika fainali za mashindano yaliyofanyika uwanja wa shule ya msingi Mvuha katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro.
Katika mashindano hayo
timu mbili mahasimu Kimelo FC na Kongwa FC wamechuana vikali ambapo Kimelo FC wameibuka mshindi kwa goli 3 kwa 2 dhidi ya Kongwa FC.
Akikabidhi zawadi hizo kwa washindi amewashukuru kwa kumaliza bila vurugu zozote na kuwasisistiza waendeleze nidhamu walioonyesha katika ligi zijazo pia.
Mh. Mfaume Amewasisitiza vijana na wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea walioshuhudia mtanange huo, "Niwaombe kwa wingi huu kujitokeza kujiorodhesha katika daftari la mpiga kura zoezi linalotarajiwa kuanza tarehe 11 Oktoba mpka tarehe 20 Oktoba 2024 ili kupata sifa ya kushiri uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024."
Kimelo FC wame jipatia zawadi nono ikiwa ni fedha taslimu shilingi 500,000 na vifaa vya michezo ikiwa ni mpira na seti ya jazzy huku mshindi wa pili Kongwa Fc wakijipatia fedha taslimu shilingi 500,000 ambapo wamekabidhiwa na mgeni rasmi Mh. Hamza Mfaume.
Ligi hii iliyoanza tarehe 11 Septemba 2024 imemalizika kwa amani ambapo jumla ya timu 8 zilishiriki chini ya uratibu wa Alice sports wear na Hanga investment na kutoa fursa ya kutangazwa kwa msimu mpya wa ligi ya MKURUGENZI CUP.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.