Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando ameutaka Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na Wakuu wa Shule kuweka mikakati ya ujenzi wa Nyumba za Walimu ili kuwawezesha kufanya kazi vizuri.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando ameyasema hayo jana Oktoba 25, 2021 alipohudhuria kikao kazi cha kuweka mikakati ya pamoja ya ujenzi wa miradi iliyopata fedha za Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19.
"Hakuna umuhimu wa kuwekeza kwenye majengo lakini tunawasahau walimu wetu, ameacha familia yake huko na kuja huku lakini basi asijutie kuja huku", amesema Mhe. Albert Msando.
Katika hatua nyingine Mhe. Albert Msando amewataka Wakuu hao wa Shule kusimamia haki za watoto na kupinga vikali vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto.
"Waambieni wakae mbali na watoto, wafanye kazi ya kufundisha watuachie watoto wetu, na Mkuu wa shule utakaezembea kusimamia hili hatutakuacha salama tutaanza na wewe", amesisitiza Mhe. Albert Msando.
Lakini pia Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Albert Msando amesema kuwa Mkuu wa Shule ambae shule yake itaongoza kwa watoto kupata mimba au kufanyiwa unyanyasaji wowote wa kijinsia basi Mkuu wa Shule huyo atakuwa hatoshi na hatobaki kwenye nafasi hiyo.
#morodcmpya
#tunatekelezakwakasiya5g
#Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.