Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amezindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 na Kuahidi kwamba Serikali itayapitia upya maslahi ya Walimu ili kuipa hadhi kada ya Ualimu.
Rais ametoa Kauli hiyo Jana Februari Mosi 2025,wakati akizindua Sera ya Elimu na Mafunzo Kwa mwaka 2014 toleo la 2023 Katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete Dodoma. Mh Rais amesema Pamoja na kuimarisha Miundombinu ya Elimu ni wakati sahihi wakuhakikisha maslahi ya Walimu yanapotiwa na kuboreshwa Kwa kuwa Mwalimu ndio nguzo Kuu ya Utekelezaji wa Sera hiyo.
"Kwa maoni yangu Mwalimu ndiye kiongozi wa Elimu hivyo Katika maboresho haya lazima Mwalimu awe katikati ya mduara wa maboresho yetu. Tutapitia upya maslahi ya kada ya Ualimu na kuipa hadhi inayostahili kama Mama wa taaluma zote Duniani"
Mh Rais ameziagiza wizara za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI),Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Wizara ya Elimu kuwezesha na kusimamia kikamilifu Utekelezaji wa Sera na mitaala mipya ili kuleta tija na matokeo yaliyokusudiwa.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.