Akizungumza katika katika uzinduzi wa kiwanda cha Sigara cha Philip Moris mjini Morogoro kilichopo katika kata ya Mkambalani, Rais Magufuli amewataka Watanzania kubadilika kwa kuwekeza katika viwanda.
“Tusirudie tena kuua viwanda Serikali itaunga mkono viwanda vyote vinavyoanzishwa. Nafahamu kuna baadhi ya vikodi kodi vinavyoleta kero, tayari nimeshatoa maelekezo kwa waziri wa viwanda kuangalia upya hizo kodi,” amesema.
“Wawekezaji tutalinda viwanda msihofu kujenga viwanda. Niwaombe viongozi wenzangu tusiwe vikwazo kwa wawekezajii kuja kuwekeza.”
Aidha, Rais Magufuli ameagiza wafanyabiashara ndogondogo wa Stendi ya Morogoro kutobugudhiwa, amchangia Shilingi laki moja mama aliyeibua kero hiyo
Katika uzinduzi huo Rais Magufuli pia amesema mashamba yote yanayofutwa wapewe wananchi bure, ni mali yao. Walidhurumiwa zamani kwa wakubwa fulani fulani kujimilikisha
Katika ziara hiyo ambapo Afande Sele (Seleman Mshidi) amejiunga na chama cha Mapinduzi akitokea ACT Wazalendo, Rais Magufuli alichukua fursa kumpongeza Afande Sele.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.