"SERIKALI imejikita kutekeleza mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi nchi nzima kwa lengo la kuibadilisha Tanzania kuwa ya kidijitali kwa kuwa anwani za makazi na postikodi ni msingi wa utambuzi wa kila mwananchi."
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonaz akimuwakilisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye wakati akifungua mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi, watendaji na wataalam wa Mkoa wa Morogoro kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi.
Dkt. Yonazi amesema kuwa anwani za makazi na postikodi ni msingi wa utambuzi ili kila mwananchi aweze kutambuliwa pale alipo ambapo nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila mtaa, barabara inakuwa na jina la mtaa na kila nyumba inakuwa na namba ya nyumba.
Pia ameitaka Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro kusimamia utekelezaji wa mfumo huu ili ifikapo Mwezi Mei mwaka huu zoezi hilo liwe limekamilika kwa kuwa utekelezaji wa mfumo huu utaiwezesha Serikali kuwa na sensa bora ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu
Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inayoratibu zoezi hilo, imeelekeza taasisi zote za Serikali nchi nzima kutekeleza mfumo huu wamiliki wote wa majengo na nyumba nao waweke namba za nyumba kwenye nyumba na majengo yao na wataalam wote waliojengewa uwezo watumike vizuri kutekeleza mfumo wa anwani za makazi na postikodi na jambo hili liwe ajenda kwenye vikao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Mariam Mtunguja akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigela amesema,
"kimsingi tumechelewa kutekeleza mfumo huu wa anwani za makazi, ila kwa kuwa viongozi mtajengewa uelewa, ni matumaini yangu kuwa kwa pamoja tutashirikiana na wataalam wetu kutekeleza jambo hili kwenye maeneo yetu ndani ya muda uliopangwa na niahidi kuwa Mkoa wa Morogoro hatutawaangusha Wizara."
Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi, amesema kuwa mfumo wa anwani za makazi na postikodi ni moja ya aina ya mawasiliano kama zilivyo aina nyingine za mawasiliano na mfumo huu unahusisha eneo husika.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.