Tanesco imetakiwa kupeleka umeme mashuleni na kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma katika maeneo hayo.
Hayo yamesemwa leo februari 17, 2022 na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro kupitia Mkutano wa Baraza la Madiwani kupitia taarifa za Kata kwa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2021/2022.
Akizungumza katika Mkutano huo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mhe. Hamisi Msangule amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. @samia_suluhu_hassan ametoa fedha nyingi na madarasa mazuri yamejengwa lakini shule hazina umeme, hivyo kupitia Mkutano huo wamemuagiza meneja wa Tanesco Wilaya ya Morogoro kuhakikisha wakati wanaendelea kusambaza umeme basi kipaumbele kiwekwe katika shule na vituo vya kutolea huduma za Afya.
Kupitia Mkutano huo pia Madiwani wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwenye Kata zao kwa kipindi cha robo ya pili ya Mwaka wa fedha 2021/2022.
#morodcmpya #tunatekelezakwakasiya5g #Kaziiendelee
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.