Timu ya viongozi na watumishi/wataalam toka Halmashari ya wilaya ya Morogoro imefanya ziara ya kikazi ndani ya Hifadhi ya taifa ya wanyama ya Selous mnamo tarehe 13/12/2017 kwa lengo la kujifunza na kujionea fursa na vivutio mbalimbali ndani ya Hifadhi hiyo.
Hifadhi ya Selous ni hifadhi kubwa barani Afrika ni mojawapo ya maeneo yenye vivutio vya kupendeza sana. Hifadhi hii ina wanyama mbalimbali wekiwemo Tembo, Mbwa Mwitu, Nyati, Viboko, Mamba, Simba pamoja na ndege aina mbalimbali.
Hifadhi hii ni kubwa sana na inapakana na mikoa mitano ya Morogoro, Pwani, Lindi Ruvuma na Mtwara. Hifadhi hii ipo upande wa kusini mwa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ikiwa imepakana na kata ya Kisaki. Hifadhi hii ina fursa nyingi zinazoweza kuisaidia Halmashauri kuongeza mapato yake ya ndani. Baadhi ya fursa ni ukusanyaji wa mapato kutokana na tozo za kodi kwa mahoteli yanayowekeza ndani ya hifadhi hiyo (service levy)
Ndani ya Hifadhi hii unatarajiwa kujengwa mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme wa Stiegler's Gorge unaotarajiwa kuzalisha umeme mkubwa Zaidi nchini Tanzania usiopungua MW2100, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro imejipanga kutumia fursa zitakazotokana na mradi huu wa kitaifa kwa ajili ya kuwaongeza pato la ndani la Halmashauri pamoja na kipato cha wananchi wanozunguka eneo la hifadhi ikiwa ni pamoja na uboreshwaji wa miundombinu wakati wa ujenzi wa Mradi.
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.