Wakuu wa idara wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Rehema S. Bwasi leo Aprili 25 wamekagua miradi ya ujenzi wa Wodi tatu za wanawake, watoto na wanaume zinazojengwa katika Hospitali yetu ya Wilaya pamoja na jengo la Utawala la Halmashauri.
Ukaguzi huo uliolengo kupata kujua maendeleo ya mradi na kujua changamoto wanazokabiliana nazo mafundi katika utekelezaji wa miradi hiyo ya Wodi hizo tatu lakini pia jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Katika hatua nyingine wakuu hao wa Idara wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wamepata wasaa wa kupokea changamoto hizo zinazowakabili mafundi na kutafuta ufumbuzi ili kazi iendelee na miradi iweze kukamilika kwa muda uliopangwa.
Ukaguzi huu unatokana na kikao cha timu ya wataalamu wa Halmashauri inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kilichoketi tarehe 24/5/2921 ambapo Mkurugenzi alitoa maelekezo kwa wakuu wa idara kutembelea miradi hiyo kwa zamu kila siku na kutoa taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo.
Aidha timu hii imetoa pia ushauri wa kihandisi pale walipoona inafaa na mafundi wamepokea ushauri kwa ajili ya utekelezaji na huu utakuwa ni utaratibu wa mara kwa mara ili kuwatia moyo mafundi na kutatua changamoto ndogondogo zinazowakabili.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.