Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mheshimiwa Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele leo Februari 23, 2025 ametembelea na kuzungumza na Maafisa Waandikishaji Wasaidizii ngazi ya Jimbo wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wakati wa Mafunzo ya Siku mbili Kwa Watendaji ngazi ya Jimbo kuhusu Uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga Kura.
Akizungumza na wanamafunzo amewataka kutumia Weledi Kwa kuwa wamefundishwa na kuelewa vyema Mafunzo hayo
"Nimatumaini yangu mmefundishwa vyema, hivyo basi tumieni Weledi wenu vizuri mtapokwenda kuwafundisha watendaji wengine" amesema Mwambigile.
Sambamba na hilo amesisitiza utunzwaji mzuri wa vifaa vinavyotumika Katika zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga Kura ili viweze kutumika Katika mzunguko mwingine ambao ni Dar-es-Salaam. Huku akiwataka pindi watakapokuwa wakiwafundisha watendaji wengine Katika Kata zao wahakikishe wazingatie Sheria,Kanuni na Taratibu za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kuleta ufanisi bora wa Zoezi hilo.
Mafunzo hayo Kwa watendaji ngazi ya Jimbo ni maandalizi ya Uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga Kura kwenye Mkoa wa Morogoro na Tanga Katika Halmashauri za Wilaya ya Bumbuli,Handeni,Pangani na Mkinga.
Zoezi hilo linatarajiwa kuanza tarehe 01-03-2025 Hadi tarehe 07-03-2025 ambapo vituo vitafunguliwa Saa 2:00 Asubuhi na Kufungwa Saa12:00 Jioni.
https://www.instagram.com/p/DGainxVq0TR/?igsh=MXMxNHJnbWJoZHIzeQ==
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.