Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Bakari Msulwa leo Juni 5, 2021 alikuwa Mgeni rasmi katika sherehe ya Siku ya Mazingira Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mvuha.
Akizungumza na Wananchi pamoja na wadau waliofika kwenye sherehe hiyo Mhe. Bakari Msulwa amesema, "Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ni mojawapo ya Halmashauri zinazokabiliwa na changamoto mbalimbali za mazingira ikiwa ni pamoja na uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji ambao unasababishwa na shughuli mbalimbali za kibinaadamu,uchomaji msitu moto,ufugaji usiozingatia utaalamu,uchimbaji wa madini usiozingatia taratibu,ukataji holela wa miti,uvamizi wa maeneo tengwa ikiwa ni pamoja na misitu ya hifadhi."
"Kwa kuzingatia kauli mbiu ya Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka huu (2021) ambayo inatutaka wanajamii kuendelea kutumia nishati mbadala kuongoa mifumo ikolojia, kimsingi kauli mbiu hii inalenga kutukumbusha ni vema jamii katika matumizi yake ya kawaida ikajielekeza zaidi kwenye matumizi mbadala ya nishati ili kupunguza mgandamizo kwenye nishati za mazao ya misitu ambazo kwa kiasi kikubwa zinachangia katika uharibifu wa mazingira ikiwemo mkaa pamoja na kuni." Amesema Mhe. Bakari Msulwa.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Mhe. Bakari Msulwa ameongezea "Tumekuwa tukisisitizwa sana na wataalam wa mazingira kutumia nishati mbadala kwa lengo la kuweka ikolojia yetu katika usawa. Na lengo la kuweka ikolojia kwa maana kila kilichopo kwenye mazingira kinahitajika kitumike kwa ustawi wa jamii bila kuharibiwa. Mfano tukitumia nishati ya gesi katika matumizi ya kawaida au ya viwanda basi tutaiacha misitu katika hali nzuri ambayo itasababisha upatikanaji wa mvua, mazalia mazuri ya wanyama pamoja na madhari nzuri kwa jamii. Hivyo matumizi ya nishati mbadala kwa lengo la kuongoa ikolojia kauli mbiu hii imekuja wakati muafaka haswa wakati serikali imeendelea kusisitiza uanzishwaji wa nishati nyingine ikiwepo umeme yote hii ni kwa ajili ya kuhakikisha ikolojia yetu inabaki katika hali ya ustawi wa jamii zetu."
Katika hatua nyingine Mhe. Bakari Msulwa ameshiriki zoezi la Uzinduzi wa Kampeni ya OKOA, WEKEZA KATIKA MAZINGIRA HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO 2021 - 2026.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.