Kivutio cha utalii maji moto ni moja ya eneo la kimkakati lililohifadhiwa kwa ajili ya kuvutia watalii na wageni mbalimbali wanaokuja kwa lengo la kufurahia mazingira ya kiutamaduni (cultural tourism) ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Eneo hili ni asilia linalotoa chemchem za Maji moto ambapo linafaa kwa kuweka Kambi za muda( campsites), kupiga picha ,kunawa na kuoga Maji ya moto kwenye chemchem za asili zinazotiririsha Maji kwa kipindi chote cha mwaka. Mvuke wa Maji moto kwenye chemchem hizi unaweza kuushuhudia vizuri nyakati za asubuhi kabla Jua kuchomoza.
Maji haya ya moto yanayotoka kwenye chemchem hizi yanasadikiwa kuwa tiba mbadala kwa kutibu magonjwa ya ngozi kama fangasi, muwasho, utangotango, mapunye ,upele, na maradhi mengineyo yakiwemo matatizo ya uzazi. .Maji haya huaminiwa kwa kuondoa mikosi na mabalaa na pia kwa wenye shida mbalimbali huyatumia maeneo haya kwa tambiko.
Wageni wengi wanapofika katika eneo hili hupendelea kutumia Maji haya kunawa uso, miguu na mikono ikiwa ni ishara ya kuomba kutatuliwa shida mbalimbali yakiwemo maradhi.
KARIBU HALMASHAURI YA WILAYA YA MOROGORO KARIBU KISAKI MAJI MOTO.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.