Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Morogoro, Mh Lucas Lemomo pamoja na timu ya madiwani hapo jana, wametembelea katika mabanda ya maonesho ya kilimo ya Halmashauri ya wilaya hiyo, yaliyofanyika katika viwanja vya maonesho ya kilimo na mifugo vya mwalimu Julias Kambarage Nyerere mjini Morogoro, na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na wananchi wa Halimashauli hiyo.
Mh Lemomo, ametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi Rehema Bwasi pamoja na timu nzima iliyohusika katika maandalizi ya maonesho hayo, kwa kujipanga vizuri katika kutoa elimu stahiki kwa wakulima, wafugaji na wafanyabiashara, ili waweze kulima na kufuga kwa kufuata kanuni na taratibu na kupata matokeo chanya na kuendeleza kukuza uchumi wa nchi.
Pia katika maonesho hayo, wananchi pamoja na wageni waliotembelea katika Halimashuri hiyo, wamefundishwa namna kuhifadhi na kuitunza milima ya Ulugulu inayopatikana katika Halmashauli hiyo namna ya kulima na kupanda miti inayotoa faida ikiemo miti ya viungo ikiwa ni njia mojawapo ya kuendelea kuitunza na kuhifadhi milima hiyo.
Rashid Athuman mkazi wa Tuliani katika wilaya ya Morogoro amefurahishwa na ukarimu wa watendakazi wa Halimashauri hiyo kwa kumfundisha juu ya kilimo endelevu cha miti ya viungo ambapo kilimo hicho kitamwezesha kulima mazao hayo pasipo kuikata miti mingine na kuharibu mazingira
Kadhalika Diwani wa kata ya Mkuyuni iliyopo katika Halimashauri hiyo Mhe Asha Ally Almasi amefurahishwa na mafunzo yaliyotolewa katika Halmashauri hiyo hasa katika sekta ya kilimo ambapo alijifunza namna ya kufuga na kulima kisasa na kupata matokeo makubwa
Aidha maadhimisho ya maonesho ya kilimo maarufu kama nanenane huadhimishwa mwezi augost kila mwaka ambapo sekta mbalimbali hukusanyika katika kila kanda na kuonesha shughuli mbalimbali wanazozifanya ikiwa ni njia mojawapo ya kujitangaza na kutoa elimu kwa wananchi na wageni wanaotenbelea maadhimisho hayo.
Maadhimisho hayo yalifunguliwa rasmi tangu August 1, 2022 na waziri mkuu mstaafu Mh Mizengo Pinda katika viwanja vya maonesho ya kilimo vya mwalimu Julias Kambarage Nyerere vilivyopo katika kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro nakuhitimishwa hapo jana August 08,2022 ambapo kitaifa maadhimisho hayo yamefanyika jijini Mbeya.
Na mwandishi Atusa Laurence Bukuku
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.