Halmashauri ya wilaya ya Morogoro kunufaika na mradi wa uwezeshaji jamii katika usismamizi endelevu wa mazao ya misitu na nishati mbadala [USEMINI]. Mradi huu unafadhiliwa na HELVETAS Swiss International kama mshirika kiongozi pamoja na CODERT na MJUMITA wenye jumla ya bajeti ya milioni 2.22Euro.
Haya yameelezwa katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro {Mvuha} na mkurugenzi wa mradi ndg. Danieni Kalimbiya ambapo amesisitiza,” Mradi utaleta mafanikio chanya kwa waadau wa mazao ya misitu haswa kwa wazalishaji, wasambazaji na wauzaji wa mkaa” Ameeleza lengo kuu la mradi ni kuhamasisha usimamizi shirikishi na endelevu wa mazao ya misitu na uzalishaji wa nishati mbadala.
Aidha mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro Ndg. Lucas Lemomo amewataka wadau wa mradi kuhakikisha wanatumiaa kipindi cha miaka mitatu kukamilisha na kutekeleza mpango kazi wa mkakati wa mradi ili kuleta tija kwa wanufaikaji. “Niwatake wataalamu mbalimbali ndani na nje ya halamashauri hii kufanya kazi kwa ushirikiano, kuongeza nguvu kwenye mpango kazi na kuwa mstari wa mbele kuhakikiksha mradi huu unatekelezeka ndani ya muda uliopangwa,” amesisitiza Ndg. Lemomo.
Nae kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro Bw. Edwin Mashala amewashukuru kwa dhati HELVETAS Swiss International, CODERT na MJUMITA kwa kuwa washirika wa mradi na kuwataka wakazi waitumie fursa hii kwa kunufaika na maendeleo ya ustawi wa mazao ya misitu, kulinda na kuepuka madhara ya mmomonyoko wa udongo na kushiriki katika kuendeleza misitu na uzalishaji wa nishati mbadala.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.