Kauli hiyo imetolewa na wazee katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe moja mwezi wa kumi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Morogoro.
Wakizungumza katika mkutano huo wazee wamesema, vijana wakiwa kama nguvu kazi ya taifa wanapaswa kuwa waadilifu na wazalendo kwa serikali na jamii kwa ujumla." Baadhi ya vijana wetu wanatukosea sana, hapo mlipo mmefikishwa kwa neema ya Mungu kupitia sisi wazee wenu, tunapoona mnakengeuka kwa serikali na jamiii tunaumia sana....." Mwenyekiti wa wazee Christopher Goliana.
Maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na utolewaji wa huduma ya upimaji wa afya bure kwa wazee na ugawaji wa neti zilizotiwa dawa ya kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Sambamba na hayo wazee wamepata fursa mbalimbali ya kupata elimu ya lishe, elimu ya usafi na utunzaji mazingira na haswa utunzaji wa vyanzo vya maji na elimu juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Mwenyekiti wa wazee Christopher Goliana ameishukuru serikali kwa jitihada inazozifanya kwa wazee hususani kwenye huduma za afya na kuiomba kuendelea kuboresha huduma hizo ili kuondoa changamoto ndogondogo zinazojitokeza haswa kwenye upatikanaji wa dawa.
Mgeni rasmi ambaye ni diwani wa kata ya Mvuha mh. Mfaume Chanzi amewapongeza wazee kwa kusherehekea siku ya wazee duniani ambapo wao wameitumia kama fursa ya kukutana na kukaa pamoja kujadili mambo mbalimbali, kupeana elimu na kujadili changamoto zinazowakabili na kuangalia namna ya kuzitatua.
Mh.Chanzi amewaomba wazee kutilia mkazo katika malezi kwa vijana, kwa kufanya hivyo kutasaidia kwa kiwango kikubwa kujenga maadili kwa jamii na kuondoa changamoto za ukiukwaji wa maadili kwa jamii ikiwa ni pamoja na vitendo vya ukatili.
Kwa upande wa utolewajiwa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji hususani mto Mvuha. Afisa mazingira wa halmashauri ndugu Joseph Ndunguru amesisitiza kuacha uchafuzi wa maji ya mto Mvuha ili kuepukana na maradhi yanayoletwa na uchafuzi wa mazingira katika vyanzo vya maji.
Akitolea ufafanuzi kuhusu utolewaji wa mikopo kwa wazee, Afisa maendeleo wa halmashauri wa wilaya ya Morogoro ndg. Florence Mwambene amesema, serikali inaendelea kuboresha utolewaji wa mikopo hiyo ambapo kuanzia sasa mikopo iliyokuwa imesimama imefunguliwa rasmi hivyo wananachi wenye sifa wanaruhusiwa kuanza kufanya taratibu za kupata mikopo.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.