Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh.Suleman Jafo (MB) leo 21/12/2017 amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na kukagua miradi miwili ya maendeleo ikiwamo mradi wa umwagiliaji wa Kiroka na Shule ya Sekondari na baadaye kukutana na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro katika ofisi za Halmashauri zilizopo eleno la Mvuha.
Akizungumza katika kikao na watumishi wa Halmashauri, Waziri Jafo amesisitiza matumizi ya Force Account katika kutekeleza miradi ya maendeleo sambamba na kutumia Tails katika ukarabati na ujenzi wa madarasa ili kupunguza adha wanazopata waalimu na wanafunzi mashuleni.
Mhe Jafu amewasisitiza watumishi kufanya kazi kwa ushirikiano na kila mtu kutimiza wajibu wake katika ujenzi wa Taifa.
Katika kikao hicho, Waziri Jafo alieleza kutoridhishwa kabisa na miradi ambayo ameitembelea, kutokana na miradi hiyo kuonesha kuwepo matumizi mabaya ya fedha za serikali. Hivyo kuahidi kuunda tume kwa ajili ya kufanya uchunguzi.
Sambamba na hilo Mhe Jafo amewataka madiwani wa Halmashauri hiyo kufahamu kwamba wao wapo kwa niaba ya wananchi hivyo wanapaswa kulinda na kusimamia rasilimali za Halmashauri hiyo.
Mhe Jafu ameahidi kurudi tena mapema mwakani ili kutembelea zaidi miradi ya maendeleo kufuatia ombi la Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Mhe. Kibena Kingo.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.