Katika kuadhimisha wiki ya huduma wa msaada wa kisheria kiwilaya tarehe 20-25/10/2019 wadau wa wanaotoa huduma za msaada wa kisheria wameshiriki katika zoezi la utoaji kutoa elimu kwa jamii kwa njia ya midahalo, matangazo, mabango na majadiliano lengo ikiwa ni kuongeza uelewa na kuongeza uhitaji wa jami juu ya msaada wa kisheria.
Wakiongozwa na Msaidizi wa huduma za msaada wa kisheria wilaya Bi Florence Mwambene Wadau hao wametoa huduma katika kata za Matombo, Mngazi na Mvuha.
Katika wiki hii Huduma zinatolewa katika kata hizo zenye Vituo 6 vya msaada wa kisheria, waelimishaji jamii vijiji 10 kwenye masuala ya Ardhi yetu, vituo nane8 vya taarifa na maarifa vya mtandao wa jinsia na pamoja na wawezeshaji toka TCRS wanashiriki katika shughuli mbalimbali za utoaji huduma na Elimu ya haki za kikatiba na msaada wa kisheria.
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.