Idara ya Afya katika Halmashauri ya wilaya ya Mororgoro imeendesha Zoezi la uchangiaji wa damu kwa hiari wilayani humu zoezi hili limefanyika mnamo tarehe February 7 na 8. Zoezi hili lilifanyika katika shule ya msingi Mvuha, eneo la Mtamba sokoni na shule ya sekondari Mvuha.
Jumla ya wanafunzi 21 walijitokeza kutoa damu katika shule ya sekondari Mvuha ambapo jumla ya Unity 18 za damu zilipatika shuleni hapo.
Katika shule ya msingi Mvuha Jumla ya wanafunzi 21 walijitokeza kuchangia damu ambapo jumla ya Unity 21 za damu zilipatikana. Zoezi hili ni endelevu na limepangwa kufanyika mara kwa mara ili kuwa na akiba ya damu ya kutosha katika wilaya kwa ajili ya kuwahudumuia wakina mama wajawazito wanaopoteza damu nyingi wakati wa kujifungua na watoto chini ya miaka 5
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake juu ya zoezi hili mwanafunzi Abdallah Juma wa kidato cha pili shuleni hapo amesema amehamasika kuchangia damu baada ya kuona vifo vya watu wengi vinaongezeka kutokana na ukoefu wa Damu unaosababishwa na, vifo vya akina mama na watoto
Mojawapo ya faida za zoezi hili ni kutokana na wanafumzi wengi kupata fursa ya kupima malaria. Uzito, Uwingi wa damu na HIV
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.