• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Baruapepe |
    • Malalamiko |
Morogoro District Council
Morogoro District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Afya
      • Maji
      • Utawala na Utumishi
      • Usafi na Mazingira
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Huduma za Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba ya Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mpango Mkakati
    • Miongozo
    • Ripoti
    • Majarida Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Maeneo ya Kihistoria

Karibu OR-TAMISEMI tuwahudumie wananchi.

Imetolewa: September 25th, 2019

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima amemkaribisha Ndg. Mathias Kabunduguru ambaye ameteuliwa kuwa Naibu katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Elimu kujiunga na Timu ya Wizara katika kufanikisha shughuli za maendeleo ya wananchi.

Akimkaribisha leo katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zilizoko Mtumba Jijini Dodoma Dkt. Gwajima amesema watumishi wa TAMISEMI wanaushirikiano wa hali ya juu na watakuwezesha kufanikisha majuku yako.

“Karibu tuchape kazi ya kuwahudumia wananchi, kwetu ni kazi tu; Sina shaka na wewe kwa kuwa ni mwalimu wangu na ulinipokea katika utumishi wa umma hivyo nakukaribisha TAMISEMI ya wananchi hivyo karibu tuwahudumie na kuwatumikia watanzania”Amesema Dkt. Gwajima.

Amewapongeza watumishi kwa weledi waliouonyesha kwa kipindi chote cha Uongozi wa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Ndg. Tixon Nzunda  katika Wizara hii mpaka alipoteuliwa na  kuwa Katibu Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

“Tumepata faraja kubwa sana kwa Ndg. Nzunda kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu na mafanikio haya ni yetu sote kwani tumefanya naye kazi nzuri zilizopelekea kuteuliwa katika nafasi ya juu zaidi ninawapongeza watumishi wote wa TAMISEMI na ninawasihi muendeleze na  kazi hii nzuri kwa Naibu Katibu Mkuu (Elimu) Ndg. Mathias Kabundunguru” Amesema  Dkt. Gwajima.

Naye Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia elimu Ndg. Kabunduguru amewataka watumishi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ,kanuni na taratibu za kazi zinavyotaka ili kuhakikisha wanatimiza adhima ya kuleta matokeo bora ya maendeleo kwa watanzania na nchi kwa ujumla.

Ndg. Kabunduguru amesema kuwa kila mmoja anawajibu wa kuheshimu kazi muda wote ili kuweza kupata matokeo chanya ambayo msingi wake ni utii wa sheria,kanuni na taratibu za kazi ili kufanyikisha malengo yanayotakiwa kwa watanzania.

“Na ili kufanikiwa kufikia malengo hayo lazima tushirikiane kwa mimi kujifunza kutoka kwenu na nyinyi kujifunza nini nilicho nacho ili kufikia adhima yetu ya kujenga taifa moja kwani sote lengo letu ni moja” Ameeleza Ndg. Kabunduguru

Naye Katibu Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu.  Mhe.Tixson Nzunda amewashukuru watumishi wa OR-TAMISEMI kwa ushirikiano waliyompa kipindi chote alipokuwa akifanya nao kazi na kutaka kuendelea kutoa ushirikiano kwa Ndg. Kabunduguru  ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake kwa ufasaha.

Aidha ikumbukwe kabla ya uteuzi wa hivi karibuni Ndg.  Kabunduguru alikuwa Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Ndg. Nzunda alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Matangazo

  • MWONGOZO WA ELIMU YA MPIGA KURA September 11, 2019
  • TANGAZO LA UCHAGUZI 2019 September 03, 2019
  • TANGAZO KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI TAREHE 07/02/2019 na 09/2/2019 January 31, 2019
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI December 14, 2017
  • Angalia zote

Habari za hivi karibuni

  • USAJILI WATOTO HALMASHAURI YA MOROGORO

    December 03, 2019
  • .

    December 02, 2019
  • .

    November 28, 2019
  • Wiki ya huduma za msaada wa kisheria

    October 23, 2019
  • Angalia zote

Video

Uunganishaji wa mimea
Vidio Zaidi

Kurasa za haraka

  • Sheria ya Manunuzi ya umma
  • Sheria ya Ardhi

Tovuti nyingine

  • Salary Slip Self Service
  • Utumishi
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Taifa
  • Tamisemi

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani yake

Wasiliana nasi

    Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road

    Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania

    Simu: +255 23 261 3185

    Simu ya Kiganjani:

    Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.