Mwenge wa uhuru unatarajia kuweka jiwe la msingi katika Mradi wa ujenzi wa Bwalo la chakula shule ya Sekondari Nelson Mandela tarehe 24//7/2018 wakati utakapokuwa katika mbio zake wilayani hapa. Ikiwa ni juhudi za serikali kuanzisha masomo ya kidato cha tano na sita wilayani hapa. Mradi huu ulianza rasmi mwezi Mei 2018 na unatarajia kukamilika katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019. Mradi huu unatekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kushirikiana juhudi za wananchi.
Mvuha Area, Mvuha - Magogoni Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.