Hospitali ya Wilaya ya Morogoro iliyopo eneo la Mvuha ambapo ndipo yalipo makao makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Morogor inatarajia kuanza kutoa huduma za matibabu kwa wananchi kuanzia tarehe 5 mwezi Oktoba, mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa mbele ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe Loata Sanare. Ambaye amefanya ziara ya siku mbili katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro
Akiwa katika eneo la ujenzi wa Hospitali hiyo mkuu wa Mkoa wa Morogoro alionekana mwenye furaha baada ya kuridhishwa na ujenzi wa Hospitali hiyo na kuwapongeza viongozi wake na kukubaliana na maamuzi yaliyopendekezwa ya hospitali hiyo kuanza kutoa huduma kwa wananchi wiki tatu zijazo baada ya majengo muhimu kukamilika.
“Niwapongeze kwa kweli kwa kazi hii, mngeenda kwa spidi hii tungekuwa tumefika mahala pazuri. Ni imani yangu kwamba ndani ya wiki tatu mlizosema tufungue hapa, wagonjwa waanzekutibiwa, hakuna cha kusubiri” alisema kwa furaha Loata Sanare.
Majengo yaliyokamilika ni pamoja na Jengo la wagonjwa wanje (OPD), Mama na Mtoto,, Jengo la kuhifadhia dawa, na Maabara. Majengo mengine yapo katika hatua mbalimbali za ukamilishwa
Mvuha Area, 450M- Bigwa-Kisaki Road
Sanduku la barua: 1880, Morogoro Tanzania
Simu: +255 23 2935458
Simu ya Kiganjani:
Barua pepe: ded@morogorodc.go.tz
Hakimiliki ©2017 H/W Morogoro. Haki zote zimehifadhiwa.